top of page

Kuhusu Mradi wa Kazi za Kijamii (CWP) 

About Community Works Project (CWP)

Mradi wa Kazi za Kijamii (CWP) ni ushirika wa mashirika sita ya kijamii ambayo yanasaidia kwa huduma za kutafuta kazi, kukuza ujuzi na kuondoa vizuizi vya  kupata ajira kwa wapokeaji wa TANF katika Kaunti ya Multomah.  Huduma zetu zinajumuisha kufunza Kiingereza kama Lugha ya Pili. 

Tunatoa huduma zifaazo kiutamaduni kwa viwango vipana vya jamii na kuwaunganisha washiriki wote kwa raslimali maalum za kijamii. 

Tunafanya kazi kwa ushirikiano wa karibu na mfadhili wetu, Oregon Department of Human Services (Idara ya Huduma za Kibinadamu ya Oregon). 

Tafadhali mwombe Mkufunzi wa Familia wako wa DHS akuelekeze kwa CWP upate usaidizi.

 

Tunapatikana katika DHS ya Kaunti ya Mashariki Kituo cha Huduma za Familia na katika Ofisi ya Uwezo wa Kujitegemea ya DHS ya Portland Kusini Mashariki. Angalia maeneo yetu. Vilevile, tunashirikiana kwa karibu na Timu za DHS za Shule katika Kaunti ya Multnomah.  

Ingawa, tovuti yetu ina upungufu wa lugha yako,tutatoa huduma zisizolipishwa za utafsiri ikiwa utazihitaji wakati unapozungumza nasi. 

Kwa raslimali zisizolipishwa za mtandaoni ambazo zinaweza kuwa muhimu kwako, tafadhali tembelea Ukurasa wetu wa Raslimali Nyingine.

bottom of page